Unknown Unknown Author
Title: LIWALE WAAGIZWA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII ILIKUPUNGUZA GHARAMA ZA MATIBABU KWA KAYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa wilaya ya Liwale,Ephrahim Mmbaga akizindua Kampeni ya Kata kwa Kata za Uhamasishaji kwa Jamii wilayani humo kujiunga na Mfuko wa A...
imageMkuu wa wilaya ya Liwale,Ephrahim Mmbaga akizindua Kampeni ya Kata kwa Kata za Uhamasishaji kwa Jamii wilayani humo kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii pamoja na kukutana na wanachama wa NHIF,,Kulia Afisa msimamizi wa Bima ya afya mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond,Kaimu Katibu Tawala wilaya na Diwani wa kata ya Liwale Bimage Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakiwa katika Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji ikiwa pamoja kuongea na wateja unaofanywa na Ofisi ya NHIF Mkoa wa Lindi
image
Mkuu wa wilaya Liwale,Mkoani Lindi,Ephraim Mmbaga ameviagiza vyama vyote vya Msingi na ushirika(AMCOS) wilayani humo kuhahakisha inawalipia wanachama wao ili waweze kuwa wanachama wa mfuko wa afya ya jamii(CHF).ili kupunguza gharama za matibabu kwa kaya.
Agizo hilo limetolewa  mjini Liwale wakati wa Uzinduzi wa  mikutano ya wadau wa mfuko wa Bima ya afya(NHIF)  na Uhamasishaji wa mfuko wa afya ya Jamii(CHF) na kupata maoni ya  jamii yatakayolenga na kujenga Utoaji na upatikanaji wa Huduma za Afya kwa mteja wa Mfuko huo ili kuwezesha Nhif  kutoa huduma iliyobora kwa wanachama wake.
Mmbaga alisema kuwa  umefika wakati kwa vyama vya msingi kuwasaidia wanachama wao kwa kuthamini na kutambua umuhimu wa kujali afya  zao ili kuwafanya  waweze kuzalisha mazao kwa wingi na kuchangia mapato kwani yanapatikana kutokana na jitihada zao.
“Ni vyema viongozi wakaona umuhimu wa kuwalipia wao  kupitia faida wanazopata kwani itawasaidia kupata matibabu kipindi cha mwaka mzima bure kwa kila Kaya  hasa wakati hali ya kifedha inapokuwa ngumu kwao”alisema Mmbaga.


Alisema kuwa hivi sasa vyama vyingi vya msingi kupitia mfumo wa stakabadhi mazao ghalani vinajipatia fedha za kutosha hivyo ni vyema wakazitumia kwa faida ya wanachama na wategemezi wao hivyo kuwa fursa pekee ya kuwahudumia wanachama kwa kugharamia matibabu yao badala ya fedha hizo kugawana posho kwenye vikao  na safari.
Alimwagiza Katibu tawala wa wilaya kukutana na viongozi wote wa vyama vya msingi ili kuweka  mkakati wa namna ya  kutekeleza agizo hilo kwa kushirikiana na viongozi wa Kata ambao ndio wapo karibu na vyama hivyo. Aidha akimalizia hotuba yake aliwataka Viongozi wa kuchaguliwa pasipo Ajira rasmi ya Serikali kuhakikisha wanashawishi wanaowaongoza
kujiunga na Mfuko huo ili kupunguza makali ya gharama za matibabu kwa kutibiwa bila Bima


Awali  Afisa msimamizi wa Bima ya afya mkoa wa Lindi,Fortunata Raymond aliwataka wanachama wa mifuko hiyo kutoa ushirikiano kwa kuwabainisha watumishi wa afya ambao kwa makusudi wanakiuka maadili ya kazi zao na kusababisha  wanachama kufanyiwa vitendo vibaya   vinavyowafanya wanachama kuichukia mifuko hiyo ambayo ndio mkombozi kwa wenye kipato duni na kwa wale  wenye kipato cha juu kulingana na ugonjwa unaomkabili.
Aidha Bi Raymond alimshukuru Diwani wa Kata ya Likongowele Wilani Liwale kwa kutambua na kuelewa huduma za Mfuko huo baada ya kufungua na kusajili duka lake katika Mfuko huo ili kusaidia huduma za Afya kwa Wananchi wake Kwa kurahisisha Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo Ofisi ya Kanda Mtwara imefungua ofisi ya Mkoa wa Lindi ambapo ipo Katika Jengo la Chama Cha Walimu Manispaa ya Lindi ambayo itatoa huduma zote zinazotolewa na  Mfuko huo

About Author

Advertisement

 
Top