Unknown Unknown Author
Title: MAANDAMANO YA WAANDISHI DAR KULAANI MAUAJI YA MWANGOSI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Waandishi wakiwa nje ya ofisi za Channel Ten jijini Dar es Salaam, kabla ya maandamano hayo Maandamano yakitoka Ofisi za Channel Ten kupiti...
Waandishi wakiwa nje ya ofisi za Channel Ten jijini Dar es Salaam, kabla ya maandamano hayoMaandamano yakitoka Ofisi za Channel Ten kupitia Morogoro RdHili ni moja ya mabango waliyokuwa nayo waandishi Ujumbe huu unaoelekezwa kwa Afande Mwema
Mwandishi Lauden Mwambona akiwa amegunga mdomo kama hivi wakati wa maandamano hayoViongozi wahahanikiza kulaani mauaji ya Mwangosi

MAANDAMANO ya Waandishi wa habari kulaani mauaji ya Mwandishi wa habari Daud Mwangosi yameingia doa baada ya waandishi kumfukuza Waziri lakini wakamkaribisha kada wa Chadema kuwahutubia.
Dosari hiyo, ilijitokeza leo, mwishoni mwa maandamano hayo kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, baada ya waandamaniji kufika wakiwa na viongozi wao wakiwemo kutoka Jukwaa la Wahariri.
Mara msafara huo ulipofika, pembezoni mwa viwanja hivyo, ukakumbana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchini alikiwa eneo hilo na mara akaungana na baadhi ya viongozi wa waandishi, ambao walijaribu kutaka kumtamtambulisha.
"Hatuatakiii, aondoke, aondoke!" waandishi wa habari kwenye maandamano hayo walipaza sauti huku wengine wakirusha mikono kuashiria kukataa kabisa waziri Nchini asizungumze lolote au kuwepo kwenye mkutano mwishoni mwa maandamano hayo.
Baadhi ya viongozi wa Jukwaa la Wahariri akiwemo Nevil Meena, walijaribu kuwatuliza waandishi lakini, ikashindikana na kwa busara Waziri Nchini akaamua kuondoka.
Hata hivyo katika kinachoonyesha kwamba kulikuwepo tofauti kati ya waandishi kuhusu kumkataa Dk. Nchini, baadhi yao walimfuata na kumhoji, lakini wengine wakaingilia kati kuzuia mahojiano hayo.
"Sasa tumesema aondoke halafu mnamhoji, mnamhoji nini na tumekataa hapa asiseme nini? mwacheni njooni kwenye mkutano wetu hapa, kwanza sijui habari hizo mtazirusha wapi, sisi ndiyo wahariri", zilisikika sauti zikipazwa.
Baada ya kuzungumza viongozi mmoja baada ya mwingine, wote wakilaani kwa nguvu zote mauaji ya Mwangosi, nayoaminika kufanywa na polisi wakati wa maandamano ya Chadema, Septemba 2, mwaka huu, mkoani Iringa, ndipo akapandishwa jukwaani Kada wa Chadema, Dk. Azaveri Rweitama.
Dk. Rweitama ambaye amewahi kushiriki shughuli nyingi za Chadema ikiwemo mikutano ya chama hicho, alipandishwa jukwaani mmoja wa viongozi wa Jukwaa la Wahariri.
"Jamani mnajua waandishi wa habari tuna marafiki. Sasa hapa tunaye Dk. Rweitama amabaye ni rafiki yetu atazungumza machache", alisema Misango akimkaribisha D. Rweitama.
Akizungumza, Reitama aliwataka waandishi wa habari kutowachukia polisi wadogo akisema, wao siyo tatizo ila tatizo ni wakubwa zao ambao alidai wanatumwa na wanasiasa kutekeleza matakwa yao.
"Sasa kama Chadema wanafungua matawi ya chama chao, kwa nini utumie polisi kuwazuia? si na wewe ukafungue matawi yako?" alisema Dk. Reitama katika moja hoja zake kwenye mkutano huo.
Kufuatia Dk. Reitama kuzungumza habari za vyama vya siasa hadi kutaja majina, baadhi ya viongozi na waandishi walianza kulauminiana kuonyesha kwamba walichofanya nin kosa.
"Sisi tulikuwa tumeshakubaliana kwamba asishirikishwe kada wa chama chochote wala wanaharakati, sasa huyu Rweitama nani amemruhusu kupanda jukwaani?, alihoji mmoja wa viongozi wa Klabu wa Waandishi wa habari wa Dar es Salaam.
Maandamano ya waandishi hao yalianzia kituo cha Channel Ten, jijini, saa tatu asubuhi, na kuendelea hadi kwenye viwanja hivyo vya Jangwani, baada ya kupitia barabara ya Morogoro.
Polisi walisindikiza maandamano hayo baadhi wakiwa nyuma na gari lao na wengine wakitembea kwa miguu, hadi kwenye viwanja hivyo, ambako halimalizika salama

HABARI HISANI YA http://habarizasiasa.blogspot.com/.

About Author

Advertisement

 
Top