NIJUZE NIJUZE Author
Title: AFRIKA GEREJI YATWAA KIKOMBE CHA CHA UJIRANI MWEMA KILICHOTOL​EWA MFUKO WA MASHIRIKA YA UMMA(PPF) - LINDI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mashindano ya Ujirani mwema Cup yaliyodhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) yamemalizika katika Manispaa ya Lindi huku...

Mashindano ya Ujirani mwema Cup yaliyodhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) yamemalizika katika Manispaa ya Lindi huku. Timu ya Afrika Garaje ikibuka kidedea baada ya kuifunga Timu ya Kusini Soccer Academy kwa Jumla ya Mabao 2 KWA 1 na kufanikiwa kutwaa kikombe
pamoja na Seti ya Jezi
Mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya Timu 8 za Manispaa ya Lindi na Kuhudhuriwa na wadau wengi wa Michezo na kushudia Timu ya Afrika gereji ikiliandama lango la Wapinzani wake karibu dakika zote za
mchezo huo.
Ni Salum Abilahi wa Afrika gereji alifanikiwa kuamsha ari ya ushindi huo baada ya kufanikiwa kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Anafi Jamvi na kuunganishwa vizuri na mfungaji huyo katika dakika ya 38 kipindi cha kwanza
Hadi Mapumziko Bao ni 1 kwa Bila….Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kuiwezesha timu ya Kusini soccer Kusawazisha bao hilo katika dakika 8 kwa njia ya Penalti baada ya Mshambuliaji wa Timu hiyo kuchezewa vibaya alipowatoka walinzi wa Afrika Gereji goli  ambalo alikudumu baada ya Anafi Selemani Jamvi kuipatiatimu yake bao la Ushindi alilofunga kwa shuti kali na kufanya  hadi Mwisho wa Mchezo Afrika gereji ikibuka mshindi na kutwaa Kombe ilo kwa mabao mawili kwa Moja

Akiongea na Blog hii kuhusiana na Mashindano hayo Meneja wa PPF kanda ya kusini-Mtwara na Lindi,Antony Ndadavala  Alieleza dhumuni la shirika lake kudhamini Michezo
ni pamoja na kujulisha jamii kuhusiana na mfuko huo ikiwemo kufunguliwa rasmi kwa ofisi ya Kanda hiyo mkoani MTWARA
Naye  Mgeni rasmi Bi Fatuma Mikidadi,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi akiongea kabla ya kufunga mashindano hayo na Kukabidhi zawadi kwa washindi alitoa wito kwa Wanasiasa pamoja na wana jamii kujitoa kusaidia Michezo katika Mkoa wa Lindi Mkoa ambao kwa miaka ya Nyuma
ulikuwa unatoa wanamichezo bora hapa Nchi Licha ya Timu hiyo ya Afrika gereji  kutwaa kikombe pia ilipata zawadi nyingine ya seti ya  jezi  huku washindi wa pili,tatu na Nne kila moja
ikijipatia seti Moja ya JEZI Huku waamuzi nao wakiambulia Tshirt na Fedha Taslimu zilizotolewa na Mfuko Huo Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Ilulu Manispaa ya Lindi.
WADAU WALIOJITOKEZA KUANGALIA FAINALI HIYO NDANI YA UWANJA WA ILULU

HABARI NA: ABDULAZIZ VIDEO...........LINDI

About Author

Advertisement

 
Top