Unknown Unknown Author
Title: ZOEZI LA SENSA NA MAKAZI LAWA ZITO, KAYA 256 ZA GOMA KUHESABIWA - KILWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kaya 256 Wilayani Kilwa Mkoani Lindi  zimetia dosari zoezi  la sensa na makazi kufuatia kaya hizo zilizo katika Kata ya kata ya Tingi, Kilwa...
imageKaya 256 Wilayani Kilwa Mkoani Lindi  zimetia dosari zoezi  la sensa na makazi kufuatia kaya hizo zilizo katika Kata ya kata ya Tingi, Kilwa Masoko na Kivinje na Njinjo wilayani himo kukataa kuhesabiwa kwa  kwa madai ya kutokuwapo kipengere cha dini katika zoezi hilo Akitoa taarifa hiyo  katika kikao cha Baraza la Maalum la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah Ulega alieleza kuwa kwa asilimia kubwa ya kaya zilizo katika wilaya zimejitokeza na kutoa takwimu zao kwa makarani waliopita katika maeneo
yao huku baadhi ya Kaya zikikataa kutoa taarifa zao


Kufuatia hatua hiyo,Ulega aliwataka Madiwani wa wilaya hiyo kuendelea kuhamasisha jamii zilizo katika zao  kujitokeza kujiandikisha katika siku zilizobaki sheria isichukue mkondo wake kufuatia ukiukwaji huo uliopo Kisheria.

Akifunga kikao cha baraza la Madiwani wa Halmashauri Hiyo,Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Ally Mohamed Mtopa aliwasihi Madiwani hao kwenda jamii zao kutoa hamasa zaidi katika siku zilizobaki huku akitupia lawama kwa baadhi ya Kaya zilizogoma kuhesabiwa kwa madai ya dini huku wakidharau maagizo ya Viongozi wao wa Dini.
Awali kikao hicho  pia kilipitishaa Sheria ndogo ndogo za kutunza rasilimali za msitu wa hifadhi wa kijiji cha Nanjirinji  Baada ya Sheria hizo kukubaliwa na kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji na baraza la maendeleo ya kata na kuwasilishwa katika kikao hicho na Mratibu  wa Shirika la  Utunzaji wa Mpingo wilayani humo.

About Author

Advertisement

 
Top