WILLIAM MALECHELA AAMUA KUWA "MWIGIZAJI WA FILAMU" BAADA YA KUSHINDWA UBUNGE WA EAC

Mtoto wa mwanasiasa mkongwe wa nchini John Malechela, William ameamua kuonesha upande wake wa pili kama muigizaji wa filamu.

William Malechela ambaye pia ni mwanasiasa, ameshiriki kuigiza kwenye filamu mpya ya Sintah, iitwayo The Return of JLO.

Kwa mujibu wa Sintah, Willam ameonesha uwezo mkubwa kwenye uigizaji wa filamu.

Mwezi April mwaka huu, William aligombea ubunge wa Afrika Mashariki lakini hakufanikiwa kuupata.

“Jana kwenye uchaguzi wa Ubunge wa EAC nimeshindwa fairly na sina malalamiko, ninawapa hongera washindi wote walioshinda leo na hasa my best friends Shyrose, Dulla, na Makongoro, Mungu awaongezee na wakatumikie vyema taifa letu!


As for me sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafakari nilipokosea na kuanza kujipanga upya,”
aliandika Willam kwenye mtandao wa Jamii Forums.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post