VIONGOZI watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi, akiwamo Mkuu wa Mkoa, Dk. Rajabu Rutengwe (aliyeketi) wametapeliwa baada ya kuambiwa kuwa wameshinda promosheni ya Airtel y sh milioni 50.
Wengine waliotapeliwa ni Katibu Tawala, Emmanuel Kalobelo na mganga mkuu, Yahya Hussein.
Ilidaiwa kuwa viongozi hao walitapeliwa kwa nyakati tofauti na watu waliojitambulisha kwao kwa njia ya simu kuwa ni watumishi wa Kampuni ya simu ya Airtel.
Tukio la kwanza lilikuwa ni la mkuu wa mkoa ambaye aliambiwa ameshinda zawadi ya sh milioni 50 na kuombwa kutuma namba za simu za watu watano alioongea nao mara ya mwisho, na mara baada ya kufanya hivyo, simu yake ikafungwa na matapeli hao.
Kwa upande wake, Dk. Yahya alisema, baada ya kupigiwa simu na matapeli hao hakuwa na shaka nao kutokana na kuwa na kauli ya busara.
Alisema baada ya kuwapa majina ya watu watano alioongea nao mara ya mwisho, aliombwa pia awatajie namba zake za siri za akaunti ya benki ya NMB ili wamtumie kiasi hicho cha fedha.
Dk. Yahya alisema kuwa aliwatumia namba hiyo kutokana na kutokuwa na shaka nao. Hata hivyo, alisema kuwa hawakuweza kumwibia fedha kutokana na akaunti yake kukosa salio la kutosha.
Kwa upande wake, Meneja wa Tawi la NMB Wilaya ya Mpanda, Erick Luhanda, alisema alipokea malalamiko kutoka kwa viongozi hao, na tayari taratibu za kibenki zimefanywa, hivyo hakutakuwa na hujuma itakayofanyika kwenye akaunti za viongozi hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.
CHANZO FREE MEDIA Zaidi soma hapa......
MATAPELI WAMTAPELI MKUU WA MKOA
Title: MATAPELI WAMTAPELI MKUU WA MKOA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
VIONGOZI watatu wa ngazi ya juu wa Serikali ya Mkoa wa Katavi, akiwamo Mkuu wa Mkoa, Dk. Rajabu Rutengwe (aliyeketi) wametapeliwa baada ya k...