NIJUZE NIJUZE Author
Title: SEMINA YA WANAHABARI KUHUSU SENSA YAFUNGULIWA MKOANI IRINGA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christine Ishengoma amewataka wanahabari kulisaidia Taifa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuendelea k...

Mkuu wa mkoa wa Iringa DKT Christine Ishengoma amewataka wanahabari kulisaidia Taifa katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi hilo.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa Rai hiyo leo katika ukumbi wa Ruco mjini Iringa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya wanahabari kutoka mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na mkoa wa Lindi na Mtwara.
Alisema kuwa zoezi hilo la sensa ya watu na mkazi lina nafasi kubwa katika Taifa ili kuwezesha kupanga bajeti kulingana na mahitaji sahihi ya wananchi wake,hivyo kuwataka wanahabari hao kusaidia kutoa elimu zaidi kwa umma .
Hivyo alisema kuwa ni wajibu kwa wanahabari kuelimishwa zaidi juu ya zoezi hilo litakavyofanyika Kama njia ya kuwezesha Taifa kufanikisha zoezi hilo.
Alisema kuwa vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau wakubwa ambavyo vinategemea zaidi Takwimu katika kufikisha ujumbe kwa Taifa hivyo ili zoezi hilo liweze kufanikiwa lazima kuwepo na ushirikiano mkubwa kutoka kwa vyombo hivyo vya habari.
DKT Ishengoma alisema kuwa hadi kufikia siku ya zoezi hilo la sensa ni siku 13 ndizo zilizosalia hivyo ni matumaini ya serikali kuona siku zilizobaki zinatumika vema katika kufikisha taarifa kwa wananchi.
Alisema kuwa sensa ya watu na makazi ni zoezi ambalo limekuwa likifanyika kila baada ya miaka 10 hivyo lazima umma kujulishwa ili kujitokeza kwa wingi katika zoezi Hilo.
Mkuu huyo wa mkoa alishauri wakuu wa kaya kuweka kumbukumbu sahihi ambazo zitawezeshwa makalani wa sensa kupata taarifa zilizo sahihi katika kufanikisha zoezi Hilo.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top