NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mkuu Gill avalia njuga Uhamisho wa RVP, kukutana na Gazidis Wikiendi hii!
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi Mtendaji wa Manchester United David Gill anatarajiwa kuingia mtamboni ili kukwamua Uhamisho wa Robin van Persie kwa kukutana na ...
DAVID_GILLMkurugenzi Mtendaji wa Manchester United David Gill anatarajiwa kuingia mtamboni ili kukwamua Uhamisho wa Robin van Persie kwa kukutana na mwenzake wa Arsenal Ivan Gazidis ili kufikia makubaliano Wikiendi hii.
Man United ilishatoa ofa mbili, za Pauni Milioni 10 na nyingine Pauni Milioni 15, lakini zote zimekataliwa bila kutolewa sababu na juzi Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, alitoboa kuhusu kukwama kwao lakini aliahidi kuendelea kumsaka Nahodha huyo wa Arsenal.
Van Persie, Miaka 29, tayari ameshaiambia Arsenal kinagaubaga kuwa anataka kuhama na angependelea kuhamia Man United na si Juventus kama ambavyo wangependelea Arsenal kwa vile hawapendi kuuza Staa wao kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu na hasa Man United ambao katika Miaka 16 ya himaya ya Meneja wao, Arsene Wenger, ndani ya Arsenal, hajauza Mchezaji hata mmoja kwa Man United.
rvp 2
Lakini, duru za ndani ya Arsenal zinadai, ikiwa Man United itaongeza Dau lao na kuzidi Pauni Milioni 20 basi Arsenal watalazimika kukubali kumuuza Van Persie ambae amebakiza Miezi 11 Mkataba wake kumalizika na, akibakia hadi mwisho na kuondoka, Klabu hiyo haitapata hata Pauni 1.
Hadi sasa, kwa ajili ya Msimu mpya, Arsenal imeshawanunua Wachezaji watatu kwa jumla ya Pauni Milioni 40 na ikimuuza Van Persie itakuwa imerudisha nusu ya gharama hiyo.
Wachezaji walionunuliwa ni Kiungo wa Spain Santi Cazorla, Straika wa France Olivier Giroud na Fowadi wa Germany Lukas Podolski.



About Author

Advertisement

 
Top