NIJUZE NIJUZE Author
Title: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB YAANZA VIBAYA-KAGAME CUP
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati Young Africans Sports Club, imeanza vibaya harakati za kutetea ubingwa wake baada...

Mabingwa watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati Young Africans Sports Club, imeanza vibaya harakati za kutetea ubingwa wake baada ya kufungwa mabao 2 - 0 na timu ya Atletico ya Burundi katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, huku washambuliaji wake wakishindwa kumalizia nafasi nzuri walizozipata na kukosa mabao ya wazi.

Huku ikionekana kuuutawala mchezo kipindi cha kwanza kwa kuwatumia viungo wake, iliweza kuwabana wapinzani wao Atletico mpaka timu zinakwenda mapumziko zilikuwa zimetoshana sare ya kutokufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Atletico kubadilisha uchezaji, walilishambulia lango la Young Africans mfululizo, lakini uimara wa walinzi wa mlinda mlango Yaw Berko ulikuwa kikwazo.

Kuumia kwa mlinzi wa kulia  Juma Abdul na kutolewa nje, kuliifanya klabu ya Young Africans kupwaya sehemu ya ulinzi kwani katika dakika ya 80 ya mchezo, Atletico walijipatia bao lao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Oliver Ndikumana  kufuatia uzembe wa walinzi hao kushindwa kuokoa hatari langoni mwao.

Atletico ilizidisha mashambulizi na katika dakika ya 90, ilijipatia bao lake la pili kupitia mshambuliaji wake Oliver Ndikumana kufuatia uzembe wa walinzi tena kushindwa kumkaba vizuri mshambuliaji wa Atletico aliyeipenya ngome na kufunga bao pili.

Hadi mpira unamalizika Atletico iimeibuka na ushindi wa mabao 2 - 0.

Kocha mkuu wa Young Africans Tom Saintfiet amewaomba wana Yanga wasife moyo, kwani bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michezo inayofuata na kuendelea na hatua zinazofuata.

Young Africans itacheza na tena siku ya jumanne na timu ya Waw Salam kutoka nchi ya Sudan Kusini ambayo katika mchezo wa leo imefungwa mabao 7-0 na timu ya APR kutoka Rwanda.

Young Africans:

1.Berko, 2.Abdul/Mbogo, 3.Luhende, 4.Cannavaro, 5.Yondan, 6.Chuji, 7.Shamte, 8.Gumbo/Nizar, Niyonzima, 9.Tegete/Bahanunzi, 10.Kiiza, 11.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top