Wananchi watakiwa kushiriki katika shughuli za maendeleo - Lindi Kilwa

image Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Peter Malekela akisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa shuguli mbali mbali za halmashauri katika maadhimisho ya Siku ya serikali za mitaa.image Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Abdallah Ulega akihutubia wananchi wa Tarafa ya Kipatimu wilayani humoimage Wananchi wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa wilaya ya kilwa

Wananchi wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kushiriki ipasavyo katika vikao mbalimbali vya serikali za mitaa ili kurahisisha Upangaji wa Mipango ya Maendeleo kufuatia hatua ya serikali kurudisha madaraka kwa ushirikiswaji kutoka ngazi ya vijiji hadi Taifa Akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya nane ya siku ya Serikali za mitaa yaliyofanyika kiwilaya katika kijiji Mtongo Kimwaga Kata ya kipatimu wilayani humo,Mkuu wa wilaya ya Kilwa ,Bw Abdallah Ulega alieleza kuwa kushiriki vema kutasaidia wilaya hiyo kupanga mipango yake shirikishi na pia jamii itatumia ipasavyo haki ya msingi kufanikisha kujenga demokrasia Awali  kaimu mkugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Peter Malekela akimkaribisha mkuu wa wilaya hiyo kuhutubia hadhara hiyo baada ya kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Zahanati ya kijiji hicho alieleza changamoto kubwa wilayani humo ipo kwa wananchi kutoshiriki kwa asilimia kubwa katika vikao mbalimbali hali inayotoa ugumu katika utekelezaji wa maamuzi yaliyoazimiwa Serikali za mitaa ni chombo kilichoundwa na kuwa na mamlaka ya kisheria huundwa na halmashauri za vijiji wilaya,Miji  na mamlaka ya miji midogo Huadhimishwa kila tarehe 01 ya mwezi wa saba ambapo pia kunawepo Burdani mbalimbali ikiwa pamoja na kutembelea na kufungua miradi mbali mbali ya jamii.

PICHA NA : ABDULAZIZ VIDEO,Kilwa

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post