DC NACHINGWEA AANZA KAZI KWA KUPATA BARAKA ZA WAZEE

image MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA,BI REGINA CHONJO
AKISIKILIZA JAMBO KWA UMAKINIFU KATIKA KIKAO CHAKE NA WAZEE WA WILAYA
HIYOimage Muasisi wa TANU NA CCM,BI KANDURU AKIMPA MKONO
MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA BI Regina Chonjo baada ya Mkuu huyo
kutembelea makazi ya Bibi huyo ambayo alipata ufadhili wa kujengewa
Nyumba hiyo na kusikitishwa na Alivyotapeliwa katika ujenzi wake

image  WAZEE WA NACHINGWEA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YAO
NA BILA KUSITA WALIDAI KUSHANGAZWA KUPATA WITO WA MKUU WA WILAYA
KUKUTANA NA WAZEE KWA KUWA KATIKA HISTORIA YAO HAWAJAWAI KUNA AU
KUSIKIA JAMBO HILO KWAOimage

image Mkuu wa wilaya mstaafu wa Bukoba ambae
alihusika na uchapaji wa viboko kwa walimu,Bw Albert Mnali akichangia
jambo ktk kikao hicho

MKUU wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo amekerwa na hali ya uchafu uliozagaa kwenye maeneo mbalimbali ya   mji wa Nachingwea na kuitaka jamii kushirikiana naHalmashauri  kujenga tabia ya usafi. Chonjo alisema kuwa licha ya kuwa na virimba katika maeneo mengi ya mji bado wananchi wanaendelea kutupa taka ovyo na kufanya kila eneo kuwa ni dampo.
“Kwa kweli hali ya mji wetu ni mbaya kwani  hata  siku ambayo nilifika niliona hali hiyo na nilishamweleza mwenyekiti wa halmashauri kuwa  hali si ya kupendeza na kumtaka kuweka  mkakati wa  kuwashirikisha wananchi” Chonjo Alisema kuwa kama watu wakishirikishwa kikamilifu wanaweza kubadilika kitabia na kujali usafi na mji wetu ukawa wa mfano kwa usafi kama ilivyo mji mingine ambayo tabia ya usafi ni ya kawaida. Kauli ya mkuu huyo wilaya aliitoa jana wakati  kizungumza na wazee wa maeneo ya mji wa  Nachingwea aliokutanao kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu kwa lengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo.  Awali  swala la hali ya uchafu uliokithiri kwenye maeneo mbali mbali ya mji wa Nachingwea lilisemwa na mmoja wa wazee hao,Albert Mnali
ambaye alisema kuwa maeneo ya yaliyo wazi yamegeuka kuwa madampo kwani kila eneo linatumiwa kutupia taka. Mnali aliisema kuwa  halmashauri imezidiwa na  taka kwani taka zinazozalishwa ni  nyingi ikilinganishwa na uwezo wa kuzisomba kwani halmashauri halina gari la kuzolea taka. Mnali aaliishauri hamashauri kumtafuta mzabuni atakayekuwa na jukumu la kuzoa taka badala ya kufanywa na halmashauri.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post