TAIFA STARZ YAPAA NAFASI 12 JUU RANK ZA FIFA

Kim Poulsen PONGEZI KWAKO; Kocha mpya Taifa Stars, Kim Poulsen kazi ya mwezi uliopita imezaa matunda

TANZANIA imependa kwa nafasi 12 kwenye orodha ya viwango vya ubora ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) iliyotolewa leo (Julai 4 mwaka huu) na shirikisho hilo.

Kwa viwango vya Juni mwaka huu, timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilikuwa namba 139 hivi sasa imefika nafasi ya 127 ikiwa na pointi 253 kulinganisha na 214 za Juni mwaka huu.

Ivory Coast inayoshika nafasi ya 16 duniani bado inaongoza kwa upande wa Afrika ikiwa na pointi 939. Timu hiyo ilikuwa katika nafasi hiyo hiyo kwa viwango vilivyotolewa Juni 6 mwaka huu. Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia ndiyo wanaoendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 1,691

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post