Wakati jana ikitangazwa kwamba mchezaji wa mpira wa kikapu,Hasheem Thabeet, ameingia mkataba wa kuichezea Oklahoma City Thunder,kwa upande wa soka barani Ulaya,kuna habari zingine za kufurahisha kwa watanzania wapenzi wa michezo kusikia kwamba mtanzania,mzaliwa wa Kikwajuni Zanzibar,Adam Nditi, ameingia mkataba wa kuanza rasmi kuwa mchezaji wa kulipwa wa timu ya kwanza ya klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza.
Nditi ambaye alizaliwa tarehe 18 September 1984 alijiunga na Chelsea Academy mwaka 2008. Mechi yake ya kwanza ilikuwa katika msimu wa 2010-11 dhidi ya Tottenham Hotspur.
Akiwa na timu ya vijana ya Chelsea, tayari Adam Nditi anacho cha kujivunia na klabu hiyo kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya vijana ya Chelsea iliyoshinda kombe la FA mwaka 2011-12.Mara zote alikuwa akiingia kipindi cha kwanza isipokuwa kwenye mechi ya fainali dhidi ya Blackburn Rovers, ambapo aliingia kipindi cha pili.
Nditi anasema mara zote amekuwa akifuatilia sana uchezaji wa Ashley Cole na kwamba mchezaji huyo ambaye sasa wataenda kucheza timu moja,ndio idol wake.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.