Ni sitofahamu iliyowakuta baadhi ya Wasanii na wananchi kwa ujumla juu ya kifo cha The greatest steven Kanumba.
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya wasanii wenzake wa filamu Steven Kanumba amefariki dunia usiku huu wa saa 9 kutokana na kupata ajali ambayo ilimpelekea kudondoka chini na kufikia kichwa usiku huu nyumbani kwake Sinza. Imethibitishwa kuwa Lulu amekatwa na yupo polisi Osterbay, mdogo wake kanumba athibitisha uwepo wa lulu wakati Kanumba akipatwa na matatizo yaliyosababisha kifo chake, anasema wawilihao walikuwa na mabishano makubwa kabla ya Lulu hajatoka ndani kumuita na kumwambia kwamba Kanumba amedondoka na anatokwa na mapovu mdomoni.
Taarifa zaidi zitaendelea kukujia kila tutakapozipata. Mwenyezi mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Steven Charles Kanumba.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.