THE GRETEST KANUMBA AFARIKI JANA USIKU.

Habari zilizotufikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam. Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho. Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa Muhimbili. Habari zaidi zitawajia baadae.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post