DIAMOND KUHUSU MPENZI WAKE MPYA.

taarifa kwa msaada wa millardayo.com

Mwimbaji Diamond Platnums amekiri kwamba kwa sasa ana mpenzi mpya ambae sio maarufu kabisa. “tuna kama mwezi hivi toka tumeanza kuwa pamoja, sio vizuri sana kumzungumzia kwa sababu naogopa sana drama mwisho yasije yakawa yale yale tena ndio maana nafanya siri lakini sio maarufu na wala sio Jokate”
millardayo.com ilipomuuliza kama ataingia tena kwenye mapenzi na mtu maarufu ambako ndiko alikotoka, Diamond amesema “kwa kweli siwezi kujua kwa sababu kila kitu kinaandikwa na mapenzi ni kama ajali”
Diamond aliwahi kukanusha exclusive on millardayo.com kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na mrembo Jokate ambae walianza kuzungumziwa sana baada ya Jokate kushuka kwenye gari moja na Diamond wakati wakiwasili kwenye show ya Mlimani City wiki kadhaa zilizopita.
Kwenye hiyo benz alishuka Diamond na mama yake mzazi pamoja na Jokate na Diamond alipoulizwa na millardayo.com alisema siku hiyo alitakiwa kushuka na mamodo wawili lakini mmoja ambae ni Lisa alishindwa kuja siku hiyo kwa hiyo ikabidi ashuke na Jokate tu.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
hii picha ilitoa ishara nyingine kwamba wawili hao wako pamoja 
kimapenzi japo wote wamekanusha kwamba hakuna chochote 
kinachoendelea kati yao.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post