Zimbabwe yaondolewa vikwazo na EU

Muungano wa Ulaya umewaondolea vikwazo baadhi ya maafisa wakuu wa serikali ya Zimbabwe, ingawa utaendelea kushikilia mali ya rais wa nchi hiyo Robert Mugabe pamoja na washirika wake wa karibu.imageKwa mujibu wa muungano huo, vikwazo vya usafiri dhidi ya mawaziri wawili viliondolewa ili kushinikiza serikali kuharakisha mchakato wa mageuzi.

Lakini msemaji wa chama cha rais Robert Mugabe,alipinga hatua hiyo akitaja vikwazo hivyo kama vinavyokiuka sheria, vyenye misingi ya ubaguzi wa rangi na vitakavyoathiri uchumi wa nchi.

Muungano huo pia uliondoa takriban kampuni ishirini za serikali kwenye orodha hiyo ambazo muungano huo ulidai kuwa zilisaidia kufadhili vurugu nchini Zimbabwe.

Ingawa Zimbabwe imepiga hatua katika mchakato wa kuunda katiba mpya, na kuimarisha uchumi, Muungano huo ungali na wasiwasi ikiwa ahadi zilizowekwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na vurugu mwaka 2008, ikiwemo ahadi za kufanyia mabadiliko idara ya polisi hazijaweza kutimizwa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post