Kuna kampuni mbili za uchimbaji wa madini ya Uranium hapa nchini, lakini hadi sasa mikabata yake hatujaiona. Tumeitaka wizara kuwasilisha mikataba hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge ili tuweze kuikagua. Kampuni ya Urinex inachimba madini hayo katika maeneo ya Manyoni(Singida) na Bahi(Dodoma) wakati Kampuni ya Mantra, inachimba Uranium katika mikoa ya Kusini. Kamati inapaswa kuhakikisha kuwa madini yanawanufaisha wananchi kuiwezesha nchi kujiingizia mapato. Kutowasilishwa kwa mikataba ya kampuni hizo, kumeifanya kamati kushindwa kujadili suala lolote kuzihusu.
SOURCE: Twitter page@JMAKAMBA
Tags
TANZANIA