C.ronaldo Aendelea kuweka rekodi - LA LIGA

image Winga wa Klabu ya Real Madrdi Cristiano Ronaldo ameendelea kuvunja rekodi katika ligi kuu ya Spain baada ya sasa kuwa ndio mchezaji aliyefunga mabao mengi katika nusu ya msimu kuliko mchezaji yeyote katika historia ya ligi hiyo.

Ronaldo alishinda tuzo ya Pichichi msimu uliopita baada ya kufunga mabao 41, na mwaka huu msimu ukiwa upo katikati mreno huyo tayari ameshatupia kambani mabao 23, na kuivunja rekodi aliyoiweka mwenyewe msimu uliopita ya mabao 22 pamoja na ile mshambuliaji wa zamani wa Barcelona Cesar ambaye nae alifunga mabao 22 katika nusu ya kwanza ya msimu wa 1950/51.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post