Uganda yaifunga Kili stars 3-1

image Katika kipindi cha nyongeza Uganda wameshinda magoli 3-1 na kupata ushindi dhidi ya Kilimanjaro Stars waliokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika michuano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 iliyofanyika leo ikiwa ni hatua ya nusu fainali. Kwa matokeo hayo Uganda itakutana na Rwanda ambayo tayari imeshakata tiketi yake baada ya kuifunga Sudan magoli 2-1 siku ya Jumamosi . Kama unavyoona hapa makocha wa timu ya Uganda walikuwa wakiwapasha misulia wachezaji wao kabla ya kuanza kipindi cha dakika 30 za nyongeza

sasa Uganda watacheza Fainali na Rwanda hapo Jumamosi, ambapo mwaka 2009 walikutana na Uganda iliibuka na ushindi wa goli 2-0 ambapo ulikuwa ushindi wao wa mara ya 11. Rwanda nayo imeingia Fainali baada ya kumtoa Sudani kwa goli 1-0.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post