SALHA ISRAEL KUCHUKUA JEEP YAKE LEO.

image MISS Tanzania 2011, Salha Israel leo ataendesha nyumbani gari toleo la kisasa aina ya Jeep, ikiwa ni zawadi yake ya kushinda taji Miss Tanzania mwaka huu.
Gari hilo lenye thamani ya sh 70milioni atakabidhiwa katika hafla fupi itakayofanyika kwenye ofisi za CFAO Motors, jijini Dar es Salaam.
Mbali na zawadi hiyo kubwa katika historia ya sanaa ya urembo nchini, malkia huyo pia ataondoka na kitita cha shilingi 8milioni.
Bosi wa Miss Tanzania kutoka Kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga alithibitisha kufanyika kwa hafla hiyo.
Lundenga alisema hafla hiyo itafanyika kuanzia saa nne asubuhi kwenye ofisi za CFAO Motors, barabara ya Pugu.
"Vodacom Miss Tanzania kesho (leo) atakabidhiwa gari lake. Ni gari jipya kwa toleo," alisema Lundenga.
Mrembo huyo alijinyakulia zawadi hiyo baada ya kuwashinda warembo wengine zaidi ya 20 katika shindano la taifa lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
Salha aliiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Miss World lilolofanyika, London nchini Uingereza na kushindwa kufua dafu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post