VODACOM MISS TANZANIA SALHA ISRAEL AKABIDHI FULANA 1000 KWA MKOA WA RUKWA NA KATAVI

image

Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi Mwangaza Msongole kulia akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa katavi litakalofanyika ijumaa katika kijiji cha makumbusho mara baada ya Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel(katikati) kumkabidhi msaada wa fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne zilizotolewa na Vodacom Tanzania, kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim.image

Vodacom Miss Tanzania 2011 Salha Israel akifurahia jambo wakati akimkabidhi fulana Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Uratibu wa Tamasha la utamaduni wa watu wa mkoa wa Rukwa na Mkoa tarajiwa wa Katavi John Kafuku, Katikati ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom imekabidhi fulana elfu moja zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi na nne kusaidia hamasa ya tamasha hilo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post