NIJUZE NIJUZE Author
Title: Swaziland yahitaji 'mabadiliko'
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kiongozi mwandamizi wa Kianglikana wa Swaziland, Askofu Meshack Mabuza, ametoa wito kwa mfalme Mswati III kuachia madaraka ya kisiasa ili ku...

imageKiongozi mwandamizi wa Kianglikana wa Swaziland, Askofu Meshack Mabuza, ametoa wito kwa mfalme Mswati III kuachia madaraka ya kisiasa ili kuipa nafasi serikali ya kidemokrasia.

Askofu Mabuza ameiambia BBC mfumo wa serikali wa "mambo ya kale" umeiingiza nchi katika mgogoro mzito wa fedha na uchumi.

Taarifa ya serikali imesema mishahara kwa wafanyakazi wa serikali yatacheleweshwa mwezi huu kutokana na upungufu wa fedha.

Mfalme Mswati, mwenye wake 13, ni kiongozi pekee mwenye kushilikia mamlaka yote kusini mwa jangwa la Sahara.

Anashutumiwa kwa kiasi kikubwa kuhusishwa na ufisadi, lakini akaahirisha sherehe zake za kufikisha miaka 25 madarakani mwaka huu kutokana na msukosuko wa fedha nchini humo.

Mpaka sasa Swaziland imekataa kupokea mkopo wa dola za kimarekani milioni 355 kutoka Afrika kusini kuisaidia kulipa gharama mbalimbali, baada ya Pretoria kuitaka nchi hiyo kufanya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top