PROFESA JAY: COMPLEX ndio amechangia nijenge nyumba hii.

image

Nyumba ya Profesa Jay, Mbezi ya Kimara DAR ES SALAAM HIPHOP LEGEND wa Bongo, ambae anazaidi ya miaka 20 kwenye muziki huo, PROFESA JAY amesema marehemu msanii COMPLEX ndio amechangia kwa kiasi kikubwa kununua kiwanja ambacho ndio amejenga nyumba anayoishi sasa hivi. J amesema “yeye ndio kila siku alikua ananiambia brother wewe ni mtu mkubwa sana unatakiwa lazima uwekeze kwenye kujenga, yule kijana kweli nitazidi kumkumbuka kila siku kwa sababu yeye ndio alinilazimisha kununua hiki kiwanja, na hata kwenye wale mashahidi wakati nanunua kiwanja, yeye ni mmoja wa walioweka sahihi, Mungu amlaze mahali pema” “hii nyumba nimeanza kuijenga wakati nimezidiwa pia na ujana mwingi, nilikua napata kiasi kikubwa sana cha fedha lakini nilikua nashindwa kumanage zile hela, kama unavyoona vijana wengi sana sasa hivi, watu wanapata sana hela, tunapata hela sana kwenye matamasha, albums, huwa tunasema sio hela zinazotosha lakini ni hela nyingi kwa mtu ambae akizihesabu, kwangu pia kusave hela lilikua tatizo kubwa sana” ameamplfy Profesa Jay Prof alianza kuijenga hiyo nyumba zaidi ya miaka mitano mpaka sasa hivi, ipo MBEZI ya KIMARA, na kitu kingine alichoongeza ni kwamba, pesa yote iliyotumika kuijenga imetokana na muziki kwa asilimia 100.

HABARI KWA HISANI YA :http://www.millardayo.com/

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post