CHUJI ARUDI NYUMBANI YANGA

image

Dirisha la usajili nchini limefunguliwa na taarifa zilizothibitishwa kutoka klabu ya Jangwani zinasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo kiungo Athumani Idd Chuji ameongezwa katika kikosi cha Yanga.

Chuji ambaye aliondoka Yanga baada ya msimu uliopita na kujiunga na Simba kabla ya kuondoka na kutaka kujiunga Villa lakini akakosa nafasi, sasa amejiunga na klabu yake ya zamani baada ya kocha Kostadin Papic kutoa mapendekezo hayo.

Pia kocha huyo wa Yanga inasemekana amewapa ruhusa ya kuondoka wachezaji Fred Mbuna na Godfrey Bonny kwa kuwa hawapo katika mipango yake ya baadae ndani ya timu hiyo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post