NIJUZE NIJUZE Author
Title: MZIZI WA FITNA KUKATWA LEO-IGUNGA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Umati mkubwa wa watu ukimsikiliza Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati akifunga ...

image

Umati mkubwa wa watu ukimsikiliza Benjamin Mkapa Rais Mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati akifunga kampeni.

image

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akiwaongoza wakazi wa mji wa Igunga na vitongoji vyake kuonyesha ishara ya kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wa mkutano wa kufunga kampeni, kwenye Uwanja wa Barafu jana.

Baada ya kampeni za takriban mwezi Mmoja zilizokuwa zimejaa kila aina ya vibweka na vituko na matukio yasiyotarajiwa ambazo hazikuwai kushuhudiwa jimboni humo na kuitimishwa kwa mbwembwe za kutimuliwa vumbi la kutosha kutoka kwa helikopta zipatazo nne hatimaye leo hii wana Igunga wataamua ni nani kati ya wagombea nane atakuwa mwakilishi wao. Jumla ya vyama nane vimesimamisha wagimbea navyo ni

  1. CCM Peter Kafumu

  2. CHADEMA – Joseph Kashindye

  3. CUF – Leopold Mahona

  4. AFP – Steven Makingi

  5. CHAUSTA – Hassan Ramadhani

  6. DP – Abdalah Chem

  7. UPDP – Hemed Ramadhan

  8. SAU – John Magifi

Kampeni za Igunga zimeshuhudia vyama vyenye nguvu ama jeuri ya pesa vikitumia kila aina ya usafiri na tambo kuwafikia wapiga kura kuanzia Mashangingi mpaka Helikopta huku vinyonge vikiishia kutumia Punda na pikipiki na hivyo kuwafikia wapigakura wachache sana achilia mbali vingine kuanza kampeni siku nne kabla ya uchaguzi.

 

Kila le kheri wana Igunga. 

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top