NIJUZE NIJUZE Author
Title: Obama aelezea mpango wa kukata matumizi
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Rais Barack Obama ametangaza mapendekezo yanayolenga kupunguza bajeti ya serikali yake kwa kipindi cha miaka kumi ijayo na kufufua uchumi wa...

Rais Barack Obama ametangaza mapendekezo yanayolenga kupunguza bajeti ya serikali yake kwa kipindi cha miaka kumi ijayo na kufufua uchumi wa nchi.

Barack Obama

Kulingana na mpango huo, serikali ya Marekani itapunguza matumizi yake kwa kiasi cha dola trilioni tatu.

Rais Obama amesema lazima matajiri nchini humo walipe viwango vikubwa vya kodi kwa mapato yao.

Lakini viongozi wa chama cha upinzani cha Republican ambacho kina wawakilishi wengi katika baraza la Congress wamepinga pendekezo la Rais Obama.

Katika hotuba iliotangazwa moja kwa moja kutoka ikulu ya White House, Rais Obama amesema ikiwa hatua hazitachukuliwa sasa mzigo huo wa madeni ya serikali utalimbikiziwa vizazi vijavyo.

"Lazima tuishi kwa kutumia kipato tulicho nacho na tupunguze matumizi ili kulipia mambo yaliomuhimu" alisema Rais Obama.

Miongoni mwa matumizi yatakayo kupunguzwa ni yale ya matibabu kwa wazee ambayo amelenga kupunguza hadi $250 bilioni.

Rais Obama hata hivyo amesema atapiga kura ya turufu kupinga juhudi zozote za kupunguza zaidi matumizi hayo ikiwa kodi hazita ongezwa.

Kiongozi wa chama cha Republican katika baraza la senate Mitch McConnell amesema mpango huo wa Rais Obama kamwe hautachochea ongezeko la nafasi za kazi na kukua kwa uchumi.

Rais Obama ameunga mkono pendekezo la mwekezaji Warren Buffet, ambapo anasema ni makosa kwa matajiri kulipa kodi sawa na wafanyikazi wao.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top