WEMA SEPETU NDANI YA CRAZY TENDANT

image

MWANADADA mwenye swaga kibao katika tasnia ya filamu Bongo Wema Sepetu, anaendelea kukimbiza katika fani hiyo ya filamu, katika mwendelezo huo anakuja na filamu inayokwenda kwa jina la “Crazy Tenant”, filamu hiyo imeandikwa na kutungwa na Selles Mapunda ‘Director of Directors’ anaongea matayarishaji wa filamu hii.

“Wema ni msanii mkubwa kwa maana ya uwezo aliokuwa nao katika fani ya tasnia ya filamu, katika filamu ya Crazy Tenant anacheza kama mhusika mkuu, nategemea wapenzi wa filamu watashuhudia uwezo wa ziada wa Wema kupitia filamu hiyo, ni filamu ambayo nimeandika kwa hisia sana, na uhusika halisi wa Wema,”anasema Mapunda.

Filamu ya “Crazy Tenant” inatarajiwa kuanza kurekodiwa kuanzia siku ya jumanne wiki ijayo , Mapunda anasema kuwa filamu hiyo itaongozwa na yeye mwenyewe, huku akitamba kuwa kwa upande wa kuchagua wasanii watakaoshiriki amefanikiwa kwa kuwapata wasanii wanaostahili.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post