NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mchezaji bora zaidi wa Uingereza Andy Murray asema kuna uwezekano wa wachezaji wa kulipwa kufanya mgomo
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Andy Murray amesema wachezaji bora zaidi wa tennis ya kulipwa wangelipenda kuona mabadiliko katika ratiba ya mapambano yao, na kuna uwezeka...

image

Andy Murray amesema wachezaji bora zaidi wa tennis ya kulipwa wangelipenda kuona mabadiliko katika ratiba ya mapambano yao, na kuna uwezekano wa kuyagomea mashindano ikiwa maslahi yao hayatatiliwa maanani.

Amesema wachezaji wengi wamekuwa wakiudhika mno kutokana na ratiba iliyosongamana, na watakutana mjini Shanghai mwezi ujao kujua hatua watakazoweza kuzingatia.

Murray amesema kwamba kuna uwezekano wa mgomo kufanyika.

"Kuna uwezekano. Nafahamu hilo, kwani baada ya kuzungumza na baadhi ya wachezaji, wao hawana wasiwasi wa kufanya hivyo [kugoma].

"Tutumaini kwamba hatutafikia hatua hiyo, lakini nina hakika wachezaji wataifikiria."

Alipoulizwa ikiwa suala hilo la mgomo litajadiliwa nchini Uchina, alijibu: "Ndio, nafikiria hivyo".

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top