NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mauaji makubwa yafanyika Burundi
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Takriban watu 36 wameuawa baada ya watu wenye silaha wasiojulikana kufyatua risasi kwenye baa iliyojaa watu karibu na mji mkuu wa Burundi, ...

image

Takriban watu 36 wameuawa baada ya watu wenye silaha wasiojulikana kufyatua risasi kwenye baa iliyojaa watu karibu na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, maafisa wamesema.

Wamesema idadi ya waliofariki dunia inaweza kuongezeka kwani watu wengi wamejeruhiwa vibaya kwenye uvamizi huo eneo la Gatumba.

Kundi la mwisho la waasi la Burundi lilisalimisha silaha zao rasmi mwaka 2009 lakini mashambulio ya hapa na pale yamekuwa yakiendelea.

Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge mjini Bujumbura amesema ni shambulio baya kabisa kutokea tangu uchaguzi kufanyika mwaka jana.

Aliyekuwa mkuu wa waasi Agathon Rwasa alijitoa kugombea urais na kukimbia baada ya chama chake cha National Liberation Forces (FNL) kuishutumu serikali kwa udanganyifu.

Serikali imelaumu mashambulio ya hivi karibuni kufanywa na magenge lakini mwandishi wetu alisema baadhi wanahofia huenda kundi jipya la waasi limeibuka.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top