NIJUZE NIJUZE Author
Title: MSHINDI WA KUHIFADHI QURAN AFRIKA APATIKANA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Jahuddin Adam...

image

Makamu wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Jahuddin Adam, kutoka Sudan, baada ya kutangazwa mshindi wa fainali hizo, zilizofanyika jijini Dar es Salaamm.

image

Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano hayo, Mohammad Sad Tawfiq, kutoka Egypt akionesha umahiri wake wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam LEO.

image

Mshiriki wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo, Kombo Bahi Makame kutoka Unguja-Tanzania, akishiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam jana, ambapo mgeni rasmi katika fainali hiyo iliyowashirikisha washiriki 14 kutoka nchi za Afrika Mashariki na kati, alikuwa ni Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.

image

Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya Viongozi wa dini ya Kiislamu, wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya kuhifadhi Qur-an, baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, Jijini Dar es Salaam.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top