NIJUZE NIJUZE Author
Title: Mbunge Mussa Hamisi Silima afariki dunia
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mbunge Mussa Hamisi Silima, aliyejeruhiwa baada ya kupata ajali jana mjini hapa, amefariki dunia.       Silima alifariki dunia leo saa tan...

image

Mbunge Mussa Hamisi Silima, aliyejeruhiwa baada ya kupata ajali jana mjini hapa, amefariki dunia.

      Silima alifariki dunia leo saa tano asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alihamishiwa na kulazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

        Taarifa za kifo cha Silima zilitangazwa jana saa 5.50 asubuhi na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wabunge wakiendelea kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2011/2012.

       "Waheshimiwa wabunge, kama mtakumbuka jana niliwatangazia kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, alipata ajali mbaya eneo la Nzuguni, ambapo mke wake, Mwanaheri Twalib alifariki dunia hapo hapo.

    "Aidha niliwaarifu kuwa, mheshimiwa Silima na dereva wake walipata majeraha makubwa na wamepelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi. Leo asubuhi kabla ya maswali,nimetoa taarifa kwenu kwamba nimeongea na mheshimiwa Silima akiwa anaendelea kupata matibabu. Ni kweli nimeongea naye.

          "Kwa masikitiko makubwa, nawatangazieni kuwa, nimepokea taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwamba, mheshimiwa Mussa Hamisi Silima amefariki dunia muda mfupi tu uliopita.

        "Kwa mujibu wa kanuni ya 149 ya kanuni za bunge, toleo la mwaka 2007, ninaahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi," alisema.

         Kufuatia msiba huo, Spika Anne aliwataka wabunge wasimame kwa dakika moja kwa heshima ya mbunge huyo.

Spika alisema kwa kipindi cha siku tatu, familia ya Silima imekumbwa na matatizo makubwa, kufuatia kutanguliwa na msiba wa kaka wa mkewe kabla ya mkewe naye kufariki dunia.

  Katika ajali iliyotokea jana eneo la Nzuguni, mke wa mbunge huyo, Mwanaheri alikufa papo hapo eneo la ajali wakati dereva wake, Chizali Sembonga, aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Corolla, lenye namba za usajili T 509 AGC alijeruhuwa.

Silima na mkewe walipatwa na ajali hiyo walipokuwa wakirejea Dodoma. Mbunge huyo alikuwa amekwenda Zanzibar kuhudhuria maziko ya kaka wa mkewe, Mwanaheri.

   Mbunge huyo na dereva wake walisafirishwa kwa ndege juzi kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu. Mwili wa Mwanaheri ulizikwa juzi alasiri.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top