HATIMAE NASRI KUTUA MAN CITY

image

Washika bunduki wa London, Arsenal leo wamekubali kumuuza Samir Nasri kwa Manchester City kwa £24million.

Nasri atasafiri kwenda Manchester leo kwa ajili ya vipimo baada ya kuachwa katika kikosi kitakachocheza na Udinese kesho.

Taarifa rasmi kutoka website ya Gunners ilisema: “Arsenal inaweza kuthibitisha kwamba wamekubaliana na Manchester City juu ya ada ya uhamisho wa Samir Nasri.

“Kiungo huyo, ambaye ametumia miaka 3 akiwa na Gunners, ameachwa katika kikosi cha Arsenal kitakachosafiri kwenda Udinese leo jioni na badala yake ataenda mjini Manchester kwa ajili vipimo.

“Uhamisho unategemea kufaulu vipimo kwa Nasri na hatua rasmi za uhamisho zitafuata.”

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post