JAQUELINE WOLPER NA MADAI YA UTAPELI

image

Jumapili iliyopita, Wolper aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa kuna mtu anatumia jina lake mtandaoni, hivyo akaomba ushauri kwa wadau.

Baada ya mahojiano alifunguka: “Ni mtu ambaye inaonekana wazi ananijua kwa undani na ananifuatilia kila hatua. Picha zangu zote anazo, mbaya zaidi anatumia jina langu kutongoza wanaume.

“Kuna mwanaume wa Kiarabu kutoka Muscat, Oman amempa huyo mtu dola 1000 (shilingi mil. 1.6). Juzi nimekutana na huyo Mwarabu Leaders Club (Kinondoni) akanichangamkia, mimi nilisalimiana naye lakini sikumjali.

“Baadaye nikashangaa watu wananifuata wakaniambia eti yule Mwarabu anadai nimekula hela zake halafu simjali. Ilibidi nimueleweshe akaelewa na siyo huyo tu, wapo wengi wamelizwa fedha kupitia jina langu.” aliishia kusema hayo. hivyo ndugu zangu mapedeshee kuweni makini….

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post