NIJUZE NIJUZE Author
Title: BONGO MUVI YANASA WENGI
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Kundi la mastaa wa filamu wa Dar es Salaam linalojulikana kwa jina la Bongo Movie linazidi kushika kasi kwa kukubalika nchini. Siku za kar...

image

Kundi la mastaa wa filamu wa Dar es Salaam linalojulikana kwa jina la Bongo Movie linazidi kushika kasi kwa kukubalika nchini.

Siku za karibuni, wasanii wanaounda kundi hilo wameanza kuingia mitaani kusaidia jamii na kuwafanya wadau wengi kuwapa tano kwa michango yao.

Kiongozi mmoja wa kundi hilo, Single Mtambalike ‘Richie’ aliweka bayana kuwa, kwa sasa kundi hilo linakwenda kijamii kwani wameanza kutoa misaada ya kibinadamu kwenye vituo mbalimbali vya kulelea watoto wasio na wazazi.

“Kwa kweli tunakwenda vizuri, tumeshakwenda kwenye vituo mbalimbali vya kulelea watoto na kutoa misaada. Naamini tunakwenda vizuri, wale wanaotuponda wameshindwa,” alisema Richie.

Aidha, aliongeza kuwa, ule ugumu waliokuwa wakiupata awali wa kuonekana ni kundi la kihuni umekwisha kwani jamii inawakubali na kutambua michango yao.

Wakati mambo yakiwanyookea Bongo Movie, taarifa zinapasha kuwa, Shirikisho la Filamu Tanzania ‘TAFF’ chini ya Mwenyekiti wake Simon Mwakifwamba lipo ‘tumbo joto’ kufuatia wasanii wake kujiunga na ‘upinzani’, Bongo Movie.

Siku za karibuni, msanii nyota Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye awali alikuwa ‘klozi’ na TAFF, sasa yuko Bongo Movie.

Msanii mwingine, Elizabeth Michael ‘Lulu’ naye ameshikika kwenye kambi hiyo huku wasanii kibao nyota, kama Maya, Steve Nyerere, Badra, Wolper, JB, Ray, Kanumba wakiwa wameota mizizi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top