WANAHABARI WAHIMIZWA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO

Wanahabari mkoani Lindi wametahadharishwa kuhusu matumizi salama ya mitandao ya kijamii ili kulinda usalama wao binafsi pamoja na kazi zao za kila siku.

Tahadhari hiyo imetolewa na mkufunzi na mwanahabari Fatma Buriani, aliyepata mafunzo maalumu chini ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya International Media Support (IMS), alipokuwa akitoa mafunzo kwa wanahabari wa Mashujaa FM mkoani humo.

Akifafanua, Buriani alisema mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa wa waandishi kuhusu namna ya kutumia mitandao ya kijamii kwa umakini zaidi, hususan wakati wanapotafuta taarifa mbalimbali mtandaoni, ili kuhakikisha usalama wao unalindwa.

Aidha, aliwakumbusha wanahabari kuepuka kufungua kila kiungo (link) kinachotumwa mitandaoni, akibainisha kuwa baadhi yake huweza kuwa na madhara makubwa na hivyo kusababisha matatizo yanayoweza kuhatarisha kazi na maisha yao.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post