![]() |
| Marie Msellemu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano -TPDC akimkabidhi kikombe kiongozi wa michezo Sekondari ya Ziwaniiliyyopo Manipsaa ya Mtwara. |
Na. Mwandishi Wetu, Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi kutoka katika shule nne za sekondari Manispaa ya Mtwara Mikindani zilizoshiriki bonanza la michezo mbalimbali wameomba waendelee kukumbukwa ili nawao vipaji vyao viweze kuonekana.
Wanafunzi hao wameyasema hayo lilipofanyika bonanza lililo andaliwa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ambao wametumia michezo kama njia ya kujenga ujirani mwema kupitia shule za sekondari zilizopo kwenye maeneo jirani na miundombinu ya gesi mkoani Mtwara.
Bonanza hilo limefanyika katika Shule ya Mangamba sekondari Mei 23, 2025 likijumuisha shule nne ambazo ni Mangamba sekondari, Msimbati na zingine ni Naliendele Sekondari na Ziwani sekondari zote zikiwa ni za manispaa ya Mtwara Mikindani.
Katika bonanza hilo timu ya Ziwani sekondari wameibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati iki-wafunga Mangamba sekondari kwa magoli manne kwa matatu baada ya mchezo huo kumalizika kwa kutoka sare ya bila kufungana.
Akifungua mashindano hayo Marie Msellemu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano -TPDC kwa niaba ya Mkurugenzi Mussa Mkame amesema lengo la bonaza hilo ni kujenga ushirikiano na undugu.
"Tumeendelea kujenga undugu na kujenga uhusiano mzuri kila linako pita bomba sisi ni majirani na nyie ni walinzi wamiundo mbinu .Tuko tayari kuona mkishindana na kupata zawadi za kigesi gesi.Tunataka kuona tunaikuza jamii na kuona mkiendelea kushirikia na TPDC"amesema Msellemu.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki bonanza hilo wameiyomba TPDC waendelee kufanya mashindano kama hayo ili waweze kuibua vipaji vya wanafunzi kupitia mashindano hayo.
Jeriani Mchopa mwanafunzi wa Mangamba sekondari ambaye alishinda kukimbiza kuku amewaomba TPDC waendelee kufanya bonanza mara kwa mara ili wanafunzi waweze kuibua vipaji vyao.
"Nashukuru kwakushinda mchezo wa kufukuza kuku hii sio mara ya kwanza nimesha wahinkushinda maranyingi niwaombe TPDC waendelee kutuletea mashindano kama haya ili tuendelee kuibua vipaji vyetu"amesema Mchopa.
"Mchezo ulikuwa wakawaida na penati hazina mwenyewe na wapinzani wetu walikuwa wa kawaida sana tunawaomba TPDC wwasiishie hapa waendelee na kwa wakati mwingine na sisi kama vijana tupo tayari kulinda miundombinu ya gesi" amesema Abdulli Uwesu mwanafuzi wa Mangamba sekondari.
Abduli Yusuphu kiongozi wa michezo shule ya msingi Ziwani amesema wamefurahishwa na ushindi huo kwani mara nyingi wanapo kutana wanatoka sare hapatikani ushindi.
"Tumefurahi sana leo kupata ushindi huu maranyingi tunapo kutana tunatoka sare ila leo tumepata ushindi tumefurahi ila tuna waomba TPDC hii isiwe mwisho tunaomba waendelee kutukumbuka kwani kuna wanafunzi wana vipaji ila hawana sehemu yakuonekana ila mashindano kama haya yatatusaidia tukaonekana"amesema Yusuphu kiongozi wa mpira Ziwani Sekondari.
Kwaupande wake mkuu wa shule ya SekondariMangamba Saidi Mpate amewashukuru TPDC kwakuandaa bonanza hilo na kuichangu shule yake kuwa wenyeji.
"Niwashukuru TPDC kwakuandaa bonanza hili nafahamu michezo ni undugu michezo ni afya na niajira.Niwaombe wanafunzi mtakao cheza mcheze muoneshe vipaji vyenu michezo ni fura.Pia niwaombe kutunza mazingira yetu yanayo tunzunguka.Bonaza hili lisiwe mwisho tunatamani liwepo na wakati mwungine na kuwe na muda wakutosho ikiwezekana hata kutwa mzima" amesema Mpate mkuu wa shule ya Mangamba.


