Chama cha Mapinduzi (CCM), kimehamasisha wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye shughuli ya kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura ili kitete nafasi ya kushika dola.
Shughuli ya uboreshaji taarifa za mpiga kura zitakazo mwenzesha kila mtanzania kupata kibali cha kutumia haki yake ya kumchagua kiongozi anayemtaka inasimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na kwa mkoa wa Dar es Salaam linatarajiwa kuanza Machi 17 hadi 23 Mwaka huu.
Akihamasisha shughuli hiyo kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Wilaya ya Ubungo, ukiwakutanisha viongozi wa Chama hicho, Jumuiya ngazi ya Shina, tawi, mitaa, Kata na Wilaya, Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla amesema ili watete dola ni lazima wafuasi wao wajiandikishe kabla ya kuanza kuwashawishi watanzania wengine.
“CCM tunawachama 12 milioni nchi nzima lakini Dar es Salaam
tunaongoza kwa idadi ya wapiga kura wengi ikilinganishwa na mikoa
mingine, tusilale mtihani tulionao kwanza kuhakikisha idadi hiyo
wanajitokeza kujiandikisha viongozi wa Wilaya, Kata, Matawi , Mitaa
hadi Shina hakikisheni watu wenu wanaenda kujiandikisha, ” amesema
Makalla.
Makalla mesema licha ya kuhitaji kutetea dola lakini uchaguzi ni namba kwani anayepata kura nyingi anatangazwa mshindi hivyo wasipuuze mchakato huo kama wanataka kuitawala nchi.