Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kuongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi Milioni 5 hadi Shilingi Milioni 10 endapo timu hizo zitafuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Simba inacheza mchezo wa marudiano leo dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano siku ya Jumapili (keshokutwa) dhidi ya Rivers United ya Nigeria katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.Simba inacheza mchezo wa marudiano
ikiwa na mtaji wa ushindi wa 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wa
robo fainali uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano ikiwa na mtaji wa ushindi wa
2-0 ilioupata ugenini huko nchini Nigeria.
Msemaji
Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
anazitakia kila la kheri Simba na Yanga na amewataka wachezaji kujituma
uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda michezo ya
kukamilisha robo fainali ili wafanikiwe kuingia nusu fainali ambapo kila
goli litakuwa shilingi Milioni 10.
Aidha,
Msigwa amesema magoli yatakayolipiwa shilingi Milioni 10 ni yale
yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya
penati.
*********************************************************************
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.