Unknown Unknown Author
Title: SIHUSIKI NA MADAWA YA KULEVYA - DITTO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii Lameck Ditto ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake "Moyo sikuma damu" amefunguka na kusema yeye hausiki na biashara y...
Msanii Lameck Ditto ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake "Moyo sikuma damu" amefunguka na kusema yeye hausiki na biashara ya dawa za kulevya wala matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amekosea kutaja jina.
Lameck Ditto
Lameck Ditto ametumia ukurasa wake wa Instagram kukanusha Taarifa hizo, amesema kuwa hata yeye amesikia jina lake likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika kesho kituo cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina lake.

"Kwenye ile Clip maarufu inayosambaa, jina langu lilitajwa kwabahati mbaya. Kulitokea makosa kwenye matamshi na walirekebisha pale pale, Binafsi sijawahi kujihusisha na hayo mavitu yanayotajwa hata siku moja. Na kwa wanaonijua vizuri wanafahamu vyema kuhusu hilo".

"Kwa hiyo natumia nafasi hii kuwasihi walioona Clip hiyo na kuwapa wasiwasi kuhusu mimi ondoeni wasiwasi huo.  Mimi siyo mmoja wao na kwa kudra za Mungu sitakuwa hivyo hata siku moja" ameandika Lameck Ditto kwenye Ukurasa wake wa Instagram
Post

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top