AJALI YAUA 7 MKOANI KILIMANJARO, WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI

Watu saba wamekufa na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo Mwika, mkoani Kilimanjaro.
Ajli Kilimanjaro
Akizungumza jana katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea saa 11. 00 jioni ikilihusisha lori, gari dogo na pikipiki.

Alisema lori hilo lilikuwa linatoka Rombo kwenda Dar es Salaam, likiwa limepakia ndizi.

“Breki za lori zilishindwa kufanya kazi na ndipo lilipoligonga gari dogo aina ya Toyota Surf lililokuwa likipishana nalo,”
alisema.

Alisema kabla ya kuanguka lori hilo pia liligonga pikipiki na taarifa za awali ni kuwa watu saba walikuwa wamepoteza maisha.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kina kuhusu majeruhi na waliopoteza maisha, alisema, “Tuko eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia majeruhi ili kuwapeleka katika Hospitali ya KCMC.”

Ajli Kilimanjaro
Habari kutoka eneo la tukio zimesema gari dogo lilikuwa mali ya kiongozi wa Chama cha Walimu mkoani humo na lilikuwa limewabeba watu watano, wakiwamo waandishi wa habari.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post