Unknown Unknown Author
Title: WALICHOSEMA TFF BAADA YA MWAMUZI SAANYA WALIYEMFUNGIA KUPEWA SHAVU NA CAF
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi wake kuhusiana na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kumteua mwamuzi Martin Saanya kuc...
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi wake kuhusiana na Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kumteua mwamuzi Martin Saanya kuchezesha mechi za kimataifa wakati amefungiwa na TFF kujihusisha na soka.
Martin Saanya
Hivi karibuni Caf ilimtangaza Saanya kuwa mmoja kati ya waamuzi watakaochezesha mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika namba 18 utakaozikutanisha Vital’O ya Burundi na Mountana ya Sudan.

Akizungumza Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema: “Saanya ni mwamuzi wa Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa), hivyo kitendo cha kufungiwa kuchezesha mechi za Ligi Kuu Bara hakiwezi kumzuia kuchezesha mechi za kimataifa ambazo zinasimamiwa wa Caf pamoja na Fifa.


“Baada ya kuvurunda katika mechi za ligi kuu tulizompatia achezeshe, tukaona hatufai, hivyo tukaamua kumweka pembeni lakini Caf wao wameona anafaa kwa sababu alifanya mtihani wao pamoja na ule wa Fifa akafanya vizuri, hivyo wana haki ya kumtumia.”

TFF ilimfungia Saanya pamoja na aliyekuwa msaidizi wake katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Samuel Mpenzu katika mchezo uliozikutanisha Simba na Yanga Oktoba Mosi, mwaka jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam baada ya kudaiwa kuvurunda mechi hiyo kwa kutoa maamuzi yenye utata likiwemo tukio la kumwonyesha kadi nyekundu Jonas Mkude wa Simba.

Pia Saanya alishindwa kutoa maamuzi sahihi juu ya bao la Yanga ambalo lilifungwa na Amissi Tambwe ambaye kabla ya kufunga alidaiwa kuushika mpira.


++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top