Unknown Unknown Author
Title: SHILOLE A.K.A SHISHI BABY AWACHANA VIJANA WANAOLALAMIKIA HALINGUMU YA MAISHA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuhena Mohammed alimaarufu kama Shilole amefunguka na kuwapa neno baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakilala...
Msanii wa muziki wa bongo fleva Zuhena Mohammed alimaarufu kama Shilole amefunguka na kuwapa neno baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakilalamika juu ya hali ngumu ya maisha huku wengi wao wakiitupia lawama Serikali ya awamu ya tano.
Zuhena Mohammed
Shilole kupitia mtandao wake wa Instgram amesema amewachana baadhi ya vijana hao na kusema wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hali ngumu ya maisha au pesa haipatikani ikiwa wao wenyewe hawahitaji kujishughulisha wamebaki kukaa vijiweni pasipo kuhangaika kutafuta mishe za hapa na pale za kuingiza kipato.

"Unalalamika hali ngumu huku umekaa" aliandika Shilole.
Shilole post
Baadhi ya mashabiki wa Shilole wamemuunga mkono kutokana na kauli yake hiyo huku wengine pia wakionyesha kutokubaliana naye wakiendelea kusema kweli maisha ya sasa ni magumu na mishe hakuna.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top