MKUU WA WILAYA AJIUZULU, AMWANDIKIA BARUA RAIS DKT MAGUFULI

Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.
Gabriel Simon Mnyele
Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.

Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu.
"Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe, kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?" Aliwahoji waandishi.

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post