VIDEO:: KWA KAULI HII BABALEVO AMEVUNJIWA HESHIMA NA SHILOLE?

December 20 ilikuwa ni maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa msanii wa Bongo Fleva mwanadada Shilole.
Shilole
Kitu ambacho kilitrend kinoma noma siku hiyo ni baada ya mwanadada Shilole kutoa kauli kumuhusu msanii mwenzake Baba Levo, kauli ambayo ilichukuliwa kama kumdhalilisha msanii mwenzake huyo.

Shilole alihojiwa katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio mchana wa siku ya birthday yake na kuulizwa kuhusu ukaribu wake na Baba Levo, ukaribu ambao unachukuliwa kama kuvuka mipaka hivi.

Ndipo Shilole akafunguka kuwa “Yani mimi nikikaaga na Baba Levo ni kama nipo na msichana mwenzangu tu, na weza kulala nae na wala asinifanye chochote.”.

Pia kwenye video hiyo utaweza kumsikia mwanadada Shilole akijibu tuhuma zinazodai kuwa yeye ana tabia ya kuwatongoza wanaume yote amefunguka kwenye video hii.


Unaweza kuplay hii video hapa chini ili kumsikia Shilole akijibu swali hilo.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post