MVUA KUBWA YAFANYA UHARIBIFU NA KUUA MTU MMOJA NA KADHAA WAJERUHIWA

Upepo na mvua kubwa vimesababisha uharibifu wa mali na miundo mbinu katika kata ya Mbebe Wilayani Ileje mkoani Songwe na kusababisha majeruhi wengi na kifo cha mtu mmoja katika kata hiyo.
Mvua Ileje
Kwa mujibu wa ripota wa globu ya jamii aliyepo wilayani humo amesema kuwa mvua za mwaka huu katika Wilaya hiyo ni chache lakini ni hatari sana kwani tukio hilo la Mvua za upepo mkali ni lapili hali inayotishia usalama wa wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkude amesema kuwa ameshafika katika eneo la tukio lilitokea janga hilo la upepo na kuzungumza na wananchi namna ya kuchukua thadhari.

"Nimewaambia wananchi wawe waungwana kwa kusaidia siku ya leo, kwani kuanzia kesho halmashauri itatoa utaratibu hata hivyo katika ajali hiyo ni mtu mmoja tu ambaye amefariki huku wengine wakiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Itumba kwa ajili ya matibabu zaidi"amesema Dc Mkude.

________________________________________
  • KIMENUKA...!! QUEEN DARLEEN NA ALIKIBA KUHUSU NGOMA YA "WAJUA"

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post