UKUMBI WAFURIKA NA KUSABABISHA WATU KUZUIWA KUINGIA NDANI SHOW YA DARASA MOSHI (+VIDEO)

Huenda huu ukawa ni wakati mzuri kuliko katika maisha yote ya muziki ya msanii Darassa CMG, kutokana na makubwa ambayo anayafanya kwasasa baada tu ya ngoma yake ya Muziki kufanya poa kinoma noma mtaani.
Darassa CMGHuwezi kuwataja wasanii ambao wanakinukisha kinoma noma kwa suala zima la shows kwasasa hapa Bongo ukaacha kumtaja Darassa. Ukiachana na mashavu ambayo alikuwa akiyapata kwenye majukwaa ya Fiesta, Darassa ni msanii ambaye ameendelea kukonga nyoyo za mashabiki kwenye kila show anayofanya.

Exclusive ambayo nataka kukupa muda huu kumuhusu mkali huyo ni show ambayo ameifanya usiku wa Christmas pande za Moshi, show ambayo taarifa zinasema kuwa ukimbi ulijaa kiasi kwamba kutoruhusiwa mtu kuingia tena ndani ya ukumbi huo (Sold Out). Ni rekodi katika historia ya muziki wa Hiphop kwa hapa kwetu Bongo.

Nakupa nafasi ya kutazama jinsi alivyofanya mkali huyo kwenye show hiyo ya Moshi.

________________________________________________________________________________
  • LIVE SHOW :: Vodacom Wasafi Festival Iringa

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post