SHILOLE KUMBE BADO MMBICHI KABISA AWEKA WAZI MAMBO USIYOYAJUA (+VIDEO)

Msanii wa muziki wa bongo fleva Shilole amefunguka na kusema kuwa mafanikio yake aliyopata kwenye muziki kama angeendelea kufanya filamu anaamini asingeweza kuyapata kabisa.
Shilole na Boycaro

Shilole akiwa na Boyfrind wake Boycaro
Shilole anasema anashukuru Mungu aliweza kumshtua mapema ili akimbie kwenye filamu na kukimbilia kwenye muziki kwani huku kwenye muziki ndiko pesa zake zilikuwepo ambazo ndani ya muda mfupi amezipata na kufanya mambo makubwa katika maisha yake.

"Namshukuru Mungu nimefikisha miaka 28 najivunia mafanikio yangu katika umri huu nilionao, nashukuru kweli kwani tayari nina bonge la mjengo na miaka yangu 28, nina watoto wawili, na biashara zingine za hapa na pale ikiwepo biashara ya chakula"
alizungumza Shilole.

MCHEKI HAPA KWENYE VIDEO CHINI.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post