Unknown Unknown Author
Title: SAD NEWS:: MCHEZAJI WA MBAO U-20, AFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKA UWANJANI KAITABA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa Mbao U-20, Ismail Mrisho Halfan akifanyiwa huduma ya kwanza ndani ya uwanja mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili. ...
Mbao Fc Vs Mwadui Fc U-20

Mchezaji wa Mbao U-20, Ismail Mrisho Halfan akifanyiwa huduma ya kwanza ndani ya uwanja mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili.

Na. Mwandishi wetu, Bukoba
Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.

Ismail Khalfan amefariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Government ya mjini Bukoba.

Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.

Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. 



Mbao Fc Vs Mwadui Fc U-20
Mchezaji Ismail Mrisho Halfan wa timu ya Mbao U-20 akitolewa uwanjani na watu wa msalaba Mwekundu baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wao uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mbao Fc Vs Mwadui Fc U-20
Mchezajiwa Mbao U- 20, Ismail Mrisho Halfan akipandishwa kwenye gari la Zimamoto baada ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa kwenye uwanja Kaitaba mjini Bukoba.
Mbao Fc Vs Mwadui Fc U-20
Gari la zimamoto klikiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera. 
(Picha na Faustine Ruta)
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top