Unknown Unknown Author
Title: RUANGWA YATAJA CHANGAMOTO ZINAZOIKABIRI MIUNDOMBINU-BARABARA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Ruangwa. Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, umetaja changamoto mbalimbali, zinazochangia kusuasua ...
Na. Ahmad Mmow, Ruangwa.
Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, umetaja changamoto mbalimbali, zinazochangia kusuasua kwa utekelezaji wa miradi, ikiwemo miundombinu ya barabara zile za vijijini, kuwa ni pamoja na kuchelewa kwa upelekaji wa fedha za matengenezo kutoka Serikali kuu.

Mwisho wa lami Kondoa
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo, Andrew Chezue wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii yaliyofanyika Ofisini kwake mjini Ruangwa.

Chezue amezitaja changamoto zingine kuwa ni baadhi ya barabara za Halmashauri ya wilaya hiyo, kutokuwa na usajili wa kisheria, fedha za barabara kutotolewa kwa wakati, pamoja na kuwepo kwa upungufu wa wahandisi na mafundi sanifu wa sekta ya ujenzi.

Zingine ni barabara zilizo nyingi ni za vumbi, hivyo uhitaji matengenezo ya mara kwa mara, inahitajika ujenzi wa madaraja na makalavati kwa wingi yanayohitajika kujengwa, ikiwemo na mifumo ya uondoaji maji, ikizingatiwa imepakana na safu ya milima ya Rondo, ambayo usababisha uwepo kwa wingi wa maji kwenye mito iliyopo ndani ya wilaya hiyo ya Ruangwa.

Mkurugenzi mtendaji huyo amesema hali ya ucheleweshaji wa upelekaji fedha katika Halmashauri hiyo na baadhi ya barabara kukosa usajili wa kisheria, jambo ambalo uzisababishia kukosa matengenezo kwa kutumia fedha zinazotokana na Mfuko wa barabara.


Chezue amesema kwa mwaka wa fedha 2016/17, Halmashauri ya Ruangwa imetengewa Jumla ya Sh 2,695,000,000.00 kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya matengenezo barabara za wilaya, vijiji na mji, lakini hadi kufikia mwezi Septemba, imeweza kupokea kiasi cha Sh 112,142,041.30 sawa na asilimia 4.2% ya bajeti iliyoidhinishiwa.

Aidha, amesema pamoja na ucheleweshwaji huo wa fedha, Halmashauri hiyo imeweza kukamilisha matengenezo ya miradi viporo ambayo ilipindukia kutoka mwaka wa fedha wa 2015 hadi 2016, ikiwa ni pamoja na kulipa madeni waliotekeleza miradi ya mwaka 2015 hadi 2016, kwa kutumia fedha zilizopokelewa kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu.

“Baada ya kupata kiasi hiki cha fedha,tumekamilisha taratibu za manunuzi za kuwapata wakandarasi wa matengenezo ya barabara zetu,na wapo katika hatua za maandalizi ya kuanza kazi”Alisema Chezue.

**********************

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top